Date: 
26-10-2022
Reading: 
Luka 18:38-43

Jumatano asubuhi 26.10.2022

Luka 18:35-43

[35]Ikawa alipokaribia Yeriko, mtu mmoja kipofu alikuwa ameketi kando ya njia, akiomba sadaka;

[36]na alipowasikia makutano wakipita, aliuliza, Kuna nini?

[37]Wakamwambia, Yesu wa Nazareti anapita.

[38]Akapiga kelele, akisema, Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu.

[39]Basi wale waliotangulia wakamkemea ili anyamaze; lakini yeye alizidi sana kupaza sauti, Ee Mwana wa Daudi, unirehemu.

[40]Yesu akasimama, akaamuru aletwe kwake; na alipomkaribia, alimwuliza,

[41]Wataka nikufanyie nini? Akasema, Bwana, nipate kuona.

[42]Yesu akamwambia, Upewe kuona; imani yako imekuponya.

[43]Mara hiyo akapata kuona, akamfuata, huku akimtukuza Mungu. Na watu wote walipoona hayo walimsifu Mungu.

Imani yako imekuponya;

Ni safari ya Yesu akielekea Yeriko, ambapo mtu kipofu alikaa kando ya njia akiomba sadaka. Aliposikia ni Yesu anapita, alimkimbilia na kuomba rehema. Alikemewa na baadhi ya watu waliokuwepo, lakini ndiyo kwanza alizidi kupaza sauti akiomba rehema. Alipoulizwa na Yesu anataka nini hakuzunguka, aliomba kupona.

Kumuita Yesu na kuomba rehema yake ilikuwa ni tendo la Imani. 

Kipofu aliposikia kuwa anayepita ni Yesu alimkimbilia na kuomba apone, ni Imani ya kweli.

Maisha yetu ya kila siku yanahitaji neema ya Mungu kufikia mafanikio. Neema hii itakaa kwetu tukidumu katika Imani.

Siku njema.