Date: 
25-04-2023
Reading: 
Matendo 20:28-31

Hii ni Pasaka 

Jumanne asubuhi tarehe25.04.2023

Matendo ya Mitume 20:28-31

28 Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.

29 Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;

30 tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.

31 Kwa hiyo kesheni, mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya kila mtu kwa machozi.

Yesu Kristo ni Mchungaji mwema;

Mtume Paulo anaongea na Wazee wa Kanisa la Efeso kuhusu kujitunza nafsi zao ili walilishe na kulitunza kundi la Mungu kama walivyoitwa. Paulo anawaambia kuwa makini na mbwa mwitu wakali ambao wangeweza kuja na kuingia kafikati yao pasipo kulihurumia kundi. Msisitizo wa Paulo ni kulichunga kundi la Mungu katika njia sahihi.

Paulo alilitaka Kanisa kusimama katika imani sahihi kwa Injili iliyokuwa imehubiriwa. Hiyo kazi ya kuelekeza watu kubaki katika njia sahihi ndiyo aliwaa wazee wa Efeso. 

Leo ujumbe huu ni wa kwetu, tusimame kama wachungaji wema tukiihubiri Injili ya kweli. Lakini yote hayo yatawezekana sote tukimtegemea Yesu Kristo aliye Mchungaji Mkuu. Sote tumfuate Yesu, maana ndiye Mchungaji mwema.

Siku njema.

Heri Buberwa 

Mlutheri