Jumatatu asubuhi tarehe 10.11.2025
Ayubu 40:1-9
1 Bwana akafuliza kumjibu Ayubu, na kusema,
2 Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi? Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye.
3 Ndipo Ayubu akamjibu Mungu, na kusema,
4 Tazama, mimi si kitu kabisa, nikujibu nini? Naweka mkono wangu kinywani pangu.
5 Nimenena mara moja, nami sitajibu; Naam, nimenena mara mbili, lakini sitaendelea zaidi.
6 Ndipo Bwana akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,
7 Jifunge viuno kama mwanamume, Mimi nitakuuliza neno, nawe niambie.
8 Je! Hata hukumu yangu utaibatilisha? Utanitia mimi hatiani, upate kuhesabiwa haki?
9 Au je! Wewe una mkono kama Mungu? Waweza kutoa ngurumo kwa sauti kama yeye?
Tuvumilie hata mwisho katika Bwana;
Biblia humsimulia Ayubu kama mtu aliyepitia mateso makali, alipoteza watoto wote, mifugo, mashamba, yaani alipoteza kila kitu. Ilifikia wakati mke wake akamshawishi Ayubu amuache huyo Mungu, Ayubu akamuita mke wake "mpumbavu". Katika yote hayo Ayubu hakutenda dhambi mbele za Mungu.
Somo tulilosoma linamuonesha Ayubu baada ya kupitia mateso akimwambia Mungu kwamba yeye si kitu, na hawezi kumjibu Mungu. Na Mungu anamhakikishia Ayubu kwamba yeye ndiye Bwana, hakuna kama yeye. Tunaona mwendelezo wa Ayubu kuvumilia katika Bwana. Nasi tuvumilie hata mwisho katika Bwana. Amina
Uwe na wiki njema yenye uvumilivu katika Bwana.
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650
