Date: 
30-11-2021
Reading: 
Wathesalonike 2:1-16

Hii ni Advent;

Jumanne asubuhi tarehe 30.11.2021

2 Wathesalonike 2:1-6

[1]Basi, ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake,

[2]kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.

[3]Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;

[4]yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.

[5]Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?

[6]Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.

Bwana analijia Kanisa lake;

Mtume Paulo katika waraka huu anakumbusha watu kudumu katika imani, pasipo kuangalia kitu chochote kilicho kinyume na neno la Mungu. Anawaasa Wathesalonike kutowafuata wale wajikwezao, wengine hadi kujiita Mungu.

Wapo wahubiri wengi siku hizi, wanaojipa utukufu kupita kiasi. Wanaona bila wao hakuna lolote laweza kufanyika, kumbe injili ni ya Yesu Kristo mwenyewe aliyelifia Kanisa kwa damu yake. Mwangalie Yesu tu, maana ndiye atakayerudi kulichukua Kanisa.

Siku njema.