DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 08 FEBRUARI, 2026

SIKU YA BWANA YA 8 KABLA YA PASAKA

NENO LINALOTUONGOZA NI

NENO LA MUNGU LI HAI

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 01/02/2026

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 01/02/2026 ni Washarika 801 na Sunday School 144

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Idara ya sanaa na michezo inapenda kuwatangazia vijana wote kuwa mazoezi ya maandalizi ya igizo la pasaka yameanza, siku za mazoezi ni jumatatu saa 11:00 jioni na Jumamosi saa 10:00 jioni, Vijana wote mnakaribishwa kushiriki maandalizi ya Igizo hili . Aidha Kutakuwa na mtihani wa ufahamu wa Biblia, vijana wote mnakaribishwa kwenye maandalizi, siku za mazoezi ni Jumanne saa 11 jioni na alhamisi saa 11jioni. Mungu awabariki sana.

8. Kwaya ya Agape wanapenda kuwashukuru washarika wote waliowashika mkono na kuungana nao kuchangia bima ya Afya kwa watoto na kuwatembelea wahitaji. Safari ya muhimbili kuwaona watoto itakua siku ya jumatano saa nane mchana wodini, pia watashiriki ibada ya maombi na wagonjwa na wahitaji itakayofanyika kanisa la KKKT Muhimbili saa 11 jioni. Wote mnakaribishwa. Ikiwa Bado ungependa kuchangia ni Acount no: 013874006021 maendeleo Bank. Mungu awabariki sana.

9. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA

 KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 14/02/2026. NDOA HII ITAFUNGWA KKKT MOSHI MJINI KATI YA

  •  Bw. Cliffson Lord Macha na Bi Karen Edmund Maeda

Matangazo mengine yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

10. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Shuma. Mtaa wa Mtitu

- Mjini kati: Hapa usharikani saa moja kamili asubuhi

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Ruth Korosso

- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Danford Mariki

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Albert Olotu

- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Henry Mwanyika

- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo.

11. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.

12. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili .

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.