DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 15 FEBRUARI, 2026
SIKU YA BWANA YA 7 KABLA YA PASAKA
NENO LINALOTUONGOZA NI
YESU AIENDEA NJIA YA MATESO YERUSALEMU
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 08/02/2026
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 01/02/2026 ni Washarika 801 na Sunday School 144
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Jumatano ijayo tarehe 18/02/2026 saa 11.00 jioni kutakuwa na ibada ya Majivu. Wazee wote watakuwa zamu.
8. Jumapili ya tarehe 01/03/2026 kutakuwa na mkutano Mkuu wa Usharika. Washarika tujiandae na kuiombea siku hiyo.
9. Idara ya sanaa na michezo inapenda kuwatangazia vijana wotekuwa mazoezi ya maandalizi ya igizo la pasaka yameanza, siku za mazoezi ni jumatatu saa 11:00 jioni na Jumamosi saa 10:00 jioni, Vijana wote pamoja na washarika wote wakubwa na wadogo wanaopenda kumtumikia Mungu kwa njia ya igizo mnakaribishwa kushiriki maandalizi ya Igizo hili . Mungu awabariki sana.
10. Maandalizi ya huduma za Wanawake katika mwezi wa Tatu:
- Tarehe 06.03.2026 MAOMBI YA DUNIA yatafanyika Kanisa Katoliki Kristo Mfalme Tabata kuanzia saa 3 asubuhi.
- Jumapili tarehe 08.03.2026 siku ya Wanawake kuongoza ibada katika Sharika na Mitaa yote ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani
- Jumatano tarehe 11.03.2026, Wanawake kurudia Kitabu cha maombi ya Dunia.
Ili tuweze kufanikisha haya yote Wanawake wote tunaombwa kukutana hapa kanisani kwa ajili ya maandalizi ya matukio yote siku ya Jumamosi ijayo tarehe 21.02.2026 saa 4 asubuhi.
11. SHUKRANI – JUMAPILI TAREHE 22/02/2026 – IBADA YA KWANZA SAA 1.10 ASUBUHI
- Jumuiya ya Upanga watamshukuru Mungu kwa ulinzi na Baraka kwa mwaka wa 2025 na neema ya kuingizwa mwaka 2026.
Neno. Zaburi 121,
- Kwaya ya Agape watamshukuru Mungu kwa mambo mengi Mungu aliyowatendea 2025, huduma ya Muhimbili kufanyika vizuri na Kujiweka mikononi mwa Mungu 2026 na mipango yote ya kwaya ikafanikiwe.
IBADA ZOTE TATU
- Wanawake wote watasogea Madhabahuni kumtolea Mungu shukrani kwa mambo mengi aliyowatendea na kuwavusha salama mwaka 2025 na kuingia 2026. Wanawake wote mnaombwa mjiandae kwa ajili ya shukrani.
12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Simbo Nkya
- Mjini kati: Hapa usharikani saa moja kamili asubuhi
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Ruth Korosso
- Kinondoni: Kwa Profesa G. Mmari
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Oysterbay na Masaki:Watashiriki ibada hapa Kanisani
13. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
14. Zamu za wazee ni kundi la Kwanza .
