DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 01 MACHI, 2026

SIKU YA BWANA YA 5 KABLA YA PASAKA

NENO LINALOTUONGOZA NI

UKATILI UPO TUUPINGE

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti. Kama kuna wageni ambao ni mara yao ya kwanza kushiriki nasi wasimame ili tuwakaribishe.

3. Matoleo ya Tarehe 22/02/2026

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 22/02/2026 ni Washarika 812 na Sunday School 254

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Jumatano ijayo tarehe 04/03/2026 saa 11.00 jioni tutaendelea na ibada ya Kwaresma. Kwaya zote zitahudumu. Wazee wote watakuwa zamu.

8. Jumapili ijyao tarehe 08/03/2026 ni siku ya Wanawake. Hivyo ibada zote siku hiyo zitaongozwa na Wanawake

9. Leo tarehe 01/03/2026 kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Usharika. Washarika wote tushiriki Mkutano huu.

10. SHUKRANI: Jumapili ijayo tarehe 08/03/2026 familia ya

  • Shelton Elton Mapesa

Watamshukuru Mungu kwa ulinzi, muongozo katika maisha yao, kuwapa kibali katika masomo, ajira, uponyaji, uzima, neema ya kukua kiroho katika maisha haya na kuwatunza tangu baba yao mpendwa alipoitwa na Bwana.

  Neno: Waefeso 5:20, Wimbo: TMW 276

11. Huduma za Wanawake katika mwezi huu wa Tatu:

- Tarehe 06.03.2026 MAOMBI YA DUNIA yatafanyika Kanisa Katoliki Kristo Mfalme Tabata kuanzia saa 3 asubuhi. Sare ni kitenge cha maombi ya Dunia.

- Jumapili tarehe 08.03.2026 siku ya Wanawake kuongoza ibada katika Sharika na Mitaa yote ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Sare ni kitenge cheupe cha KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

- Jumatano tarehe 11.03.2026. Wanawake kurudia Kitabu cha maombi ya Dunia. Sare ni kitenge chetu kipya cha Kiharaka. Wanawake wote tunaombwa kuhudhuria katika matukio yote bila kukosa. Mungu awabariki.

12. Jumapili ya tarehe 12/04/2026 katika ibada zote tatu tutampongeza Mch. Charles Mzinga pamoja na familia yake kwa kipindi alichotumika hapa Kanisa Kuu Azania Front. Jumuiya zote, Vikundi vyote na Washarika wote mnaombwa kujiandaa kwa ajili ya siku hiyo. Mungu awabariki.

13. Umoja wa Vijana wa Usharika wa Azania Front wameandaa mapumziko ya pamoja ya vijana (mtoko) yanayoenda kwa jina la Nguvu Retreat chini ya idara ya ustawi wa kijana tarehe 14/03/2026, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika kituo cha mapumziko Tonymax (Tonymax Park) kilicho Mwembe Mdogo, Kigamboni. Neno la siku ni Maisha Yaliyotimilika Kupitia Vipawa Vyako (Fulfilled Life Through Your Gifts); 1 Petro 4:10. Kujiandikisha kujiunga katika mtoko wasiliana na Uongozi wa umoja wa vijana

14. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Kinyaha

- Mjini kati: Hapa usharikani saa moja kamili asubuhi

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Korosso

- Kinondoni: Kwa Hilda Lwezaula

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Elihanan na Mwl. Caroline Lema

- Ilala, Chang’ombe, Buguruni:, Oysterbay na Masaki:, Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach:, Watashiriki ibada hapa Kanisani

15. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.

16. Zamu: Zamu za wazee ni Wazee wote .

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.