Date: 
16-08-2022
Reading: 
2Timotheo 2:14-19

Jumanne asubuhi 16.08.2022

2 Timotheo 2:14-19

[14]Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wasikiao.

[15]Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.

[16]Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu,

[17]na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto,

[18]walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha wa kadha.

[19]Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, 

Bwana awajua walio wake. 

Na tena, 

Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu.

Hekima ituingizayo mbinguni;

Mtume Paulo anamwandikia Timotheo juu ya muumini anayekubaliwa na Mungu kuwa ni yule mwenye kunena maneno ya faida. Maneno yasiyo na faida ni yale yasiyosaidia watu kumpokea Yesu. Kumbe ujumbe wa Paulo hapa ni neno la Mungu kuhubiriwa kwa usahihi wake. Na katika hilo, wote wanaagizwa kumcha Bwana, msisitizo ukiwa kila alitajaye jina la Bwana kuacha uovu. 

Sisi tunawajibika kujiuliza kama tunakubalika na Mungu, yaani kama tunanena maneno yenye faida. Tujihoji kama tunasimama kusema ukweli wa neno la Mungu, lakini pia kama tunaishi kwa maelekezo ya neno la Mungu. Sisi tunalitaja jina la Bwana, sasa tuache uovu.

Siku njema.