MATANGAZO YA USHARIKA 

 TAREHE 16 APRILI, 2023  

NENO LINALOTUONGOZA  NI

YESU KRISTO AJIFUNUA KWA WANAFUNZI WAKE 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Kuna mgeni mmoja aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 09/04/2023

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwa kumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi jioni saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. 

5. Uongozi wa shule ya jumapili unawaomba wazazi kuwaleta Watoto siku ya jumamosi saa 7.00 mchana kwajili ya mazoezi ya maandalizi ya Tamasha la uimbaji ngazi ya jimbo.

6. Kwaya Kuu ya Usharika wapo Lushoto kwaajili ya Mkutano Mkuu wa Kwaya. Pia watashiriki Ibada Kanisa Kuu Lushoto. Washarika tuwaombee.

7. NDOA.

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 05/05/2023.

SAA 08.00 MCHANA HAPA USHARIKANI

Bw. EMMANUEL ABRAHAMU MWANYAMAKI na Bi.ELIZABETH BUGALAMA

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 29/04/2023.

SAA 08.00 MCHANA

BW. RAMON KARIM NAWAB Na BI. LULU NANCY ISHENGOMA

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

7. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Oysterbay na Masaki: Kwa MAMA MOSHI

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo:  

Kwa MZEE EVATT KUZILWA 

- Mjini kati: Kwa ………………………………..

- Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Kwa ……………………………..

- Kinondoni: Kwa BW PROFESA MMARI  

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa …………………..

- Upanga: Kwa BW & BI SABAYA

- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach:Kwa ……………………………

- Tababa: Kwa………………………………….

- English Service: Kwa ………………………………………….

8. MAHUDHURIO IBADA YA JUMAPILI ILIYOPITA 09/04/2023

JUMLA IBADA ZOTE WATU WAZIMA NI 1,046

SHULE YA JUMAPILI 321

9. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yet

u, Bwana ayabariki.