Date: 
28-04-2023
Reading: 
Ezekiel 34:15-16

Hii ni Pasaka 

Ijumaa asubuhi tarehe 28.04.2023

Ezekieli 34:15-16

15 Mimi mwenyewe nitawalisha kondoo zangu, nami nitawalaza, asema Bwana MUNGU.

16 Nami nitawatafuta waliopotea, nitawarudisha waliofukuzwa, nitawafunga waliovunjika, nitawatia nguvu wagonjwa; nao wanono na wenye nguvu nitawaharibu; nitawalisha hukumu.

Yesu Kristo ni mchungaji mwema;

Viongozi katika Israeli waliongoza watu vibaya. Walitanguliza maslahi binafsi, hawakuwajali watu wao. Mungu alitumia mfano wa Mchungaji (viongozi) na kondoo (watu) kuonesha ambavyo hakufurahia ambavyo watu waliongozwa. Somo la asubuhi hii linaonesha Bwana akiahidi kuwalisha kondoo wake. Atawatafuta waliopototea, atawarudisha waliofukuzwa, atawafunga waliovunjika na kuwaponya wagonjwa.

Mungu alikemea tabia ya kuongoza watu wake vibaya, akaahidi kuwaongoza watu wake mwenyewe. Kwa hiyo hapa Mungu anaahidi kuwa kiongozi (Mchungaji) wa watu (kondoo) wake. Ahadi hii inaishi hata leo, maana Yesu Kristo ndiye Mchungaji mwema. Mwamini yeye uokolewe.

Siku njema.

 

Heri Buberwa