MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 04 MEI, 2025
SIKU YA BWANA YA 2 BAADA YA PASAKA
NENO LINALOTUONGOZA NI
YESU NI MCHUNGAJI MWEMA
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia na cheti. Kama kuna wageni ambao ni mara yao ya kwanza kushiriki nasi wasimame ili tuwakaribishe.
3. Matoleo ya Tarehe 27/04/2025
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 27/04/2025 ilikuwa ni washarika 661. Sunday School 248.
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Leo tarehe 04/05/2025 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.
8. Uongozi wa Umoja wa Vijana unapenda kuwatangazia vijana wote juu ya uanzishwaji wa programu endelevu ya maombi ya vijana. Program hii itahusisha maombi ya mfungo, semina za maombi, kambi za maombi na mikesha ya maombi. Ratiba ya mwaka imetangazwa kupitia group la WhatsApp ambapo Alhamisi ya tarehe 8 Mei vijana wote mnakaribishwa kushiriki maombi ya mfungo. Utaratibu wa maombi haya umetangazwa pia kupitia group la WhatsApp. Kama Kijana haupo kwenye group unaweza kumuona kiongozi yoyote wa vijana au kijana mwenzako aliye kwenye group akuunganishe. Pia uongozi unapenda kuwatangazia vijana wote kuwa maandalizi ya kushiriki mtihani wa ufahamu Biblia ngazi Jimbo unaotarajiwa kufanyika tarehe 17/05/2025 yameanza. Hivyo vijana wote wanakaribishwa kujumuika katika maandalizi hayo. Muda wa maandalizi hayo ni kila siku ya Jumatatu na Jumatano saa 12 jioni na Jumamosi saa 9 alasiri.
9. Umoja wa vijana Azania Front kupitia idara yake ya Ustawi wa kijana inawatangazia vijana kuwepo kwa Webina (Semina ya mtandaoni). Siku ni Jumatano tarehe 07/05/2025 saa 2.00 usiku hadi saa 3.00 usiku. Linki ya kujoin webina itasambazwa kupitia kundi la Whatsapp la Umoja wa vijana.
10. Jumapili ijayo tarehe 11/05/2025 ni siku ya ubatizo wa watoto wadogo na kurudi kundini. Watakao hitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.
11. Familia ya Bwana na Bibi Heri Buberwa wamepata zawadi ya mtoto wa kiume jumapili tarehe 27/04/2025 katika hospitali ya Taifa Muhimbili. Baba, Mama na Mtoto wanaendelea vizuri.
12. SHUKRANI: Jumapili ijayo tarehe 11/05/2025 katika ibada ya Kwanza saa 1.00 asubuhi.
- Nancy Lawrencia Gregory atamshukuru Mungu kwa kumbukumbu ya kuzaliwa tarehe 11/05
Neno: Zaburi 23:1 Wimbo: TMW 135
14. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 24/05/2025
NDOA HII ITAFUNGWA KKKT MBEZI BEACH KATI YA
-
Bw. Elimsiri Edwin Ngowi na Bi. Evelyne George Biita
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 10/05/2025
SAA 7.00 MCHANA
-
Bw. Gilbert Bryson Mshanga na Bi. Jacqueline Samora Kihwele
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa Matangazo karibu na duka letu la vitabu.
16. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Kavugha
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Adv Joseph na Adv. Vupe Mpuya
- Kinondoni: Kwa Profesa Geofrey Mmari.
- Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
- Oysterbay/Masaki: Kwa ………………..
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa……………………………..
- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Kwa Mama Theudas Msangi
17. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.]
18. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.