Date: 
30-05-2025
Reading: 
Yohana 16:21-22

Ijumaa asubuhi tarehe 30.05.2025

Yohana 16:21-22

21 Mwanamke azaapo, yuna huzuni kwa kuwa saa yake imefika; lakini akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena ile dhiki, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni.

22 Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye.

Kristo amepaa katika Utukufu wake;

Bwana Asifiwe;

Kabla ya neno hili nyuma kidogo, Yesu alikuwa amewaambia wanafunzi wake kuwa bado kitambo kidogo hamnioni, na bado kitambo kidogo mtaniona. Hawakumuelewa, lakini alikuwa anaongelea habari za kufa na kufufuka kwake na kupaa mbinguni. Alikuwa anawapa ujumbe ambao ulikuwa unaonesha kwamba wangepatwa na huzuni, lakini hiyo huzuni yao ingekuwa furaha.

Katika kuelezea huzuni hiyo kugeuka furaha, ndipo katika somo Yesu anatoa mfano wa mwanamke aonaye huzuni saa yake ya kuzaa ikifika, lakini akiisha kuzaa mwana hujawa na furaha. Kumbe Yesu alikuwa anawaambia wanafunzi kuwa baada ya kupitia mateso yote na kufufuka, angepaa kurudi mbinguni na wanafunzi wake wangejaa furaha tele. Tujawe na furaha katika Kristo maana amepaa mbinguni kutuandalia makao. Amina

Ijumaa njema 

 

Heri Buberwa