Date: 
31-05-2025
Reading: 
Warumi 8:34

Jumamosi asubuhi tarehe 31.05.2025

Warumi 8:34

Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.

Kristo amepaa katika Utukufu wake;

Mtume Paulo anahoji kwamba Mungu akiwa upande wetu, ni nani aliyeko juu yetu? Kwamba yeye aliyemtoa mwanae afe kwa ajili ya dhambi zetu awezaje kutuacha? Somo linakazia kwamba Kristo mfufuka katika wafu ndiye Mwokozi wetu, tena ndiye hutuombea. Mkazo wa Paulo. Msisitizo wa Mtume Paulo ni kuwa hakuna jambo lolote liwezalo kututenga na Kristo.

Hatuwezi kutengwa na Kristo tukibaki katika imani kama tulivyompokea. Hiyo ni ahadi yake, kwamba hatatuacha. Mtume Paulo asubuhi hii anatukumbusha ahadi hii ya kutotengwa na Kristo, ambayo ni ya hakika ili tusimuache Yesu Kristo. Tukimshika Yesu Kristo hatutengwi naye, lakini zaidi anatupa uzima wa milele. Amina

Jumamosi njema

Heri Buberwa