Jumamosi asubuhi tarehe 06.09.2025
Wafilipi 2:5-11
5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
Mungu huwapinga wenye kiburi;
Mtume Paulo anawaandikia Wafilipi kuuiga unyenyekevu wa Kristo. Anasema nia ya unyenyekevu iliyokuwa ndani ya mioyo yao ibaki hivyo hivyo. Anawataka kuuiga mfano wa Yesu aliyejifanya kuwa hana utukufu, akawa mtumwa akiwa mfano wa wanadamu. Paulo anaendelea kusema kuwa Yesu alinyenyekea akawa mtii hata mauti ya msalaba. Paulo anaonesha ukuu wa Mungu kwa watu wote, ambaye kwake kila goti litapigwa.
Ujumbe wa mtume Paulo kwetu leo ni kuuiga mfano wa Yesu aliyekuwa mnyenyekevu na mtii, hata mauti ya msalaba. Tunaelekezwa kuwa wanyenyekevu katika maisha yetu ya kila siku, tukiamini katika ukuu wa Mungu ambaye kwake kila goti litapigwa. Tuache kiburi. Amina
Jumamosi njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650