Date: 
27-09-2025
Reading: 
Matendo ya mitume 9:10-19

Jumamosi asubuhi tarehe 27.09.2025

Matendo ya Mitume 9:10-16

10 Basi palikuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana.

11 Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba;

12 naye amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, na kumwekea mikono juu yake, apate kuona tena.

13 Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemu;

14 hata hapa ana amri itokayo kwa wakuu wa makuhani awafunge wote wakuitiao Jina lako.

15 Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.

16 Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.

Tunaitwa kuwa mawakili wa Mungu;

Sauli alikuwa akilitesa sana Kanisa kwa kuwatesa waamini, kuwafunga na wengine kuwaua (22:3-5). Katika sura ya 9 alikuwa njiani kuendelea na mateso yake juu ya waaminio, ndipo akakutana na Yesu Kristo aliyemtokea na kumwambia kwamba alimuudhi kwa kuwatesa watu wake. Alianguka, wasaidizi wake wakawa hawaoni kitu bali sauti ikiyokuwa ikiongea naye. Alipoamka wakampeleka Dameski. 

Somo la leo asubuhi linaanzia hapo, ambapo Anania anatumwa na Bwana nyumbani kwa Yuda, huko akamwekee mikono Sauli ili apate kuona tena. Anania alikataa akisema taarifa za Sauli hazikuwa nzuri, maana aliwatesa watu wa Mungu. Bwana akamwambia aende, maana huyo Sauli alikuwa chombo kiteule kwa ajili ya Injili. 

Anania aliitikia wito kama tunavyosoma hapa chini;

Matendo ya Mitume 9:17-19

17 Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.
18 Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa;
19 akala chakula, na kupata nguvu. Akawa huko siku kadha wa kadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski.

Ujumbe wa siku;

1. Anania aliitika wito wa Bwana kwenda Dameski nyumbani kwa Yuda kumwekea mikono Sauli. Naweza kusema alienda kumweka wakfu. Tunaitwa kutumia vipawa vyetu kumtumikia Bwana pasipo uvivu na visingizio.

2. Sauli huyu ndiye alikuja kuwa Paulo (13:9) alipotokewa na Yesu aliitika, tayari kwa Injili. Baadaye alianza kuhubiri Injili, Jumapili iliyopita tuliona akisema yeye ni mtumishi na wakili wa siri za Mungu. Tunaalikwa kuwa mawakili wema katika utume wetu. Amina

Jumamosi njema

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com