Date: 
29-09-2025
Reading: 
Waamuzi 13:8-9

Jumatatu asubuhi tarehe 29.05.2025

Waamuzi 13:8-9

8 Ndipo huyo Manoa akamwomba Bwana, akisema, Ee Bwana, nakuomba, yule mtu wa Mungu uliyemtuma na aje kwetu mara ya pili, atufundishe hayo yatupasayo kumfanyia huyo mtoto atakayezaliwa.

9 Mungu akasikiza sauti ya Manoa; naye malaika wa Mungu akamwendea yule mwanamke tena alipokuwa anaketi shambani; lakini mumewe, Manoa, hakuwapo pamoja naye.

Tuwapende na kuwajali watoto katika Bwana;

Bwana Asifiwe;

Somo la asubuhi hii ni sehemu ya mwanzo wa historia ya Samsoni. Ukisoma kuanzia mstari wa kwanza, mke wake Manoa ambaye alikuja kuwa mama yake Samsoni alitokewa na Malaika akapewa habari njema kuwa atachukua mimba na atazaa mtoto mwanamume. Bila shaka ilikuwa habari njema na ya furaha sana maana mwanamke yule alikuwa tasa. Malaika alimwambia yule mwanamke kwamba mtoto huyo angekuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni hata siku ya kufa kwake. 

Ukiendelea kusoma unaona tangazo la kuzaliwa mtoto mwanamume likipokelewa, na mtoto alizaliwa akaitwa jina lake Samsoni. Leo hatumuongelei Samsoni na yaliyotokea, bali Manoa na mke wake waliomtegemea Mungu akawapa mtoto katika hali ya utasa. Na zaidi, mtoto ambaye alikuwa mnadhiri wa Mungu.

Watoto tulio nao ni zawadi toka kwa Mungu. Hivyo tumshukuru kwa zawadi hii ya watoto, na tuwafundishe kumjua yeye aliye njia ya kweli na uzima. Amina

Uwe na wiki njema ukiwapenda na kuwajali watoto.

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com