DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 14 DESEMBA, 2025

SIKU YA BWANA YA 3 KATIKA MAJILIO

NENO LINALOTUONGOZA NI

ITENGENEZENI NJIA YA BWANA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 07/12/2025

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 07/12/2025 ni Washarika 595 Sunday School 175

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia wazazi/walezi kuwaandikisha watoto waliofika umri wa kuanza mafundisho ya Kipaimara. Atakaye hitaji kumuandikisha mtoto afike ofisi ya Parish Worker.

8. NDOA: HAKUNA NDOA ZA WASHARIKA

Lakini matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

9. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mzee Evatt Kuzilwa

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa …..

- Mjini kati: Watatangaziana

- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi Kelvin Matandiko

10.  Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.

11. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.