DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 21 DESEMBA, 2025

SIKU YA BWANA YA 4 KATIKA MAJILIO

NENO LINALOTUONGOZA NI

TUTAZAMIE KWA FURAHA UJIO WA MWOKOZI

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 14/12/2025

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 07/12/2025 ni Washarika 909 Sunday School …

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia wazazi/walezi kuwaandikisha watoto waliofika umri wa kuanza mafundisho ya Kipaimara. Atakaye hitaji kumuandikisha mtoto afike ofisi ya Parish Worker.

8. Mafundisho ya ubatizo yatafanyika siku ya tarehe 23/12/2025 kwanzia saa 9 Alasiri

9. Jumapili ijayo tarehe 28/12/2025 tutashiriki chakula cha Bwana. Washarika tujiandae.

10. Shukrani: Jumapili ijayo tarehe 28/12/2025 katika ibada ya tatu saa 4.30 asubuhi familia tatu zitamshukuru Mungu

  • Mama Vicky Makani pamoja na familia watamshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyowatendea na anayoendelea kuwatendea, pamoja na Mama Vicky Makani kukumbuka siku yake ya kuzaliwa tarehe 28/12.

 

  • Washarika waliozaliwa mwezi December (Team December) jumapili ya tarehe 28/12/2025 katika ibada ya tatu watamtolea Mungu shukrani ya pekee.

Neno: Zaburi 23:1-6, Wimbo: TMW 168 Beti la 3

  • Familia ya Bwana na Bibi Yusuph Elieza pia watamshukuru Mungu kwa matendo makuu Mungu aliyowatendea, Kutimiza mwaka mmoja wa Ndoa pamoja na kumponya mke Highiness.

 Neno: Zaburi 23, Wimbo: Toka kwaya ya Vijana (Namshukuru Mungu)

11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo …..

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: …………..…..

- Kinondoni: Kwa ……………….

- Mjini kati: ………………

- Oysterbay, Masaki: Kwa ………………

- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa ………………….

- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: …………………………………….

12. RATIBA YA SIKUKUU.

 Jumatano Tarehe 24/12/2025 ibada zitakuwa mbili

- Saa 11.00 jioni ibada ya Kingereza.

- Saa 1.00 Usiku ibada ya Kiswahili.

Alhamisi Tarehe 25/12/2025 ibada zitakuwa tatu

- Saa 1.00 asubuhi ibada ya Kiswahili

- Saa 3.00 asubuhi ibada ya Kingereza

- Saa 4.30 asubuhi ibada ya Kiswahili

Ijumaa Tarehe 26/12/2025 ibada itakuwa moja

- Saa 2.00 asubuhi ibada ya Kiswahili itaambatana na Kipaimara pamoja na ubatizo wa watoto.

 Jumatano Tarehe 31 ibada zitakuwa mbili

- Saa 11.00 jioni ibada ya Kingereza

- Saa 1.00 usiku ibada ya Kiswahili

Alhamisi Tarehe 01/01/2026 ibada zitakuwa mbili

- Saa 2.00 asubuhi ibada ya Kiswahili

- Saa 6.00 mchana ibada ya Kingereza

13. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.