Yaliyojiri Ibada ya PASAKA - Azaniafront

Akitoa neno la siku Baba Askofu, Dkt. Alex Malasusa alisema kuwa ufufuo wa Yesu Kristo ni ishara tosha juu ya uweza mkuu wa Mungu, na kwamba uweza wake huo hauwezi kuzuiwa na jambo lolote. “Kama Yesu asingefufuka basi imani yetu ingekuwa bure. Inawezekana mpaka leo kuna watu hawaelewi maana ya ufufuo japokuwa wanasherehekea Pasaka na kujazana makanisani. Ufufuo wa Yesu Kristo sio tu suala la kihistoria bali ni suala ambalo ni endelevu katika maisha yetu ya kila siku,” alisema Baba Askofu Malasusa.

Yaliyojiri Ibada ya Ijumaa Kuu - Azaniafront

Akitoa neno la siku ya Ijumaa Kuu, Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dean Chediel Lwiza aliwaasa washarika kuitumia siku hiyo kutafakari matendo yao na kumrudia Mungu. “Ijumaa Kuu kama tunavyoiita sisi wakristo ni siku ya huzuni sana kwetu kwani Yesu tunayemtaja kila siku alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Hivyo sisi wakristo wa leo tuna deni kubwa kwake. Ijumaa Kuu sio tu siku ya kumbukumbu, inabidi ibadilishe kitu katika maisha yetu ya kila siku,” alisema Dean Lwiza.