Date: 
06-04-2020
Reading: 
John 3:22-30 (Yohana 3:22-30)

MONDAY 6TH APRIL 2020   MORNING                                                                      

John 3:22-30 New International Version (NIV)

22 After this, Jesus and his disciples went out into the Judean countryside, where he spent some time with them, and baptized. 23 Now John also was baptizing at Aenon near Salim, because there was plenty of water, and people were coming and being baptized. 24 (This was before John was put in prison.) 25 An argument developed between some of John’s disciples and a certain Jew over the matter of ceremonial washing. 26 They came to John and said to him, “Rabbi, that man who was with you on the other side of the Jordan—the one you testified about—look, he is baptizing, and everyone is going to him.”

27 To this John replied, “A person can receive only what is given them from heaven. 28 You yourselves can testify that I said, ‘I am not the Messiah but am sent ahead of him.’ 29 The bride belongs to the bridegroom. The friend who attends the bridegroom waits and listens for him, and is full of joy when he hears the bridegroom’s voice. That joy is mine, and it is now complete. 30 He must become greater; I must become less.”

Humility stems from understanding who God is and who we are in His presence. Humility stems from understanding that everything I am and have has been entrusted to me by God to be used for His purpose and glory.

As Christians, we must constantly battle pride and grow in humility. Moreover, if we think we have attained any measure of humility, we have to be on guard against being proud of our humility.


JUMATATU TAREHE 6 APRILI 2020   ASUBUHI                                          

YOHANA 3:22-30

22 Baada ya hayo Yesu na wanafunzi wake walikwenda mpaka nchi ya Uyahudi; akashinda huko pamoja nao, akabatiza.
23 Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa.
24 Maana Yohana alikuwa hajatiwa gerezani.
25 Basi palitokea mashindano ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi mmoja juu ya utakaso.
26 Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ng'ambo ya Yordani, yeye uliyemshuhudia, tazama, huyo anabatiza na watu wote wanamwendea.
27 Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lo lote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni.
28 Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nalisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake.
29 Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi.
30 Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.

Unyenyekevu hutokea pale tunapoelewa Mungu ni nani; na nafasi yetu mbele zake. Unyenyekevu huja kwa kuelewa kuwa, jinsi nilivyo na kila kitu nilicho nacho nimepewa na Mungu ili kutumika kwa kusudi na utukufu wake.

Sisi kama Wakristo, daima tunahitaji kupambana na kiburi ili tuzidi kukua katika unyenyekevu. Zaidi ya hayo, ikiwa tutadhani kuwa tumefikia kipimo chochote cha unyenyekevu, basi na tujilinde tusiwe na kiburi juu ya unyenyekevu huo.