Matangazo ya Usharika tarehe 27 April 2025

MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 27 APRILI, 2025

SIKU YA BWANA YA 1 BAADA YA PASAKA

NENO LINALOTUONGOZA NI

YESU AJIFUNUA KWETU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia na cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 20/04/2025

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

IBADA: Washarika Azania Front Cathedral Waadhimisha Alhamisi Kuu 2025

Katika ibada ya Alhamisi Kuu iliyofanyika katika Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral, 17 Aprili 2025 na kuongozwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ambaye pia ni Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Baba Askofu Dkt. Alex Malasusa iliwakutanisha washarika na wageni mbalimbali kukumbuka siku ambayo mwokozi wetu Yesu Kristo alisalitiwa na mmoja wa wanafunzi wake aliyejulikana kama Yuda Iskarioti na hivyo kupelekea kukamatwa, kuteswa msalabani mpaka kufa kwake.