Date: 
28-04-2020
Reading: 
John 6:1-14 (Yohana 6:1-14)

TUESDAY 28TH APRIL 2020   MORNING                                                                     

John 6:1-14 New International Version (NIV)

1 Sometime after this, Jesus crossed to the far shore of the Sea of Galilee (that is, the Sea of Tiberias), and a great crowd of people followed him because they saw the signs he had performed by healing the sick. Then Jesus went up on a mountainside and sat down with his disciples. The Jewish Passover Festival was near.

When Jesus looked up and saw a great crowd coming toward him, he said to Philip, “Where shall we buy bread for these people to eat?” He asked this only to test him, for he already had in mind what he was going to do.

Philip answered him, “It would take more than half a year’s wages[a] to buy enough bread for each one to have a bite!”

Another of his disciples, Andrew, Simon Peter’s brother, spoke up, “Here is a boy with five small barley loaves and two small fish, but how far will they go among so many?”

10 Jesus said, “Have the people sit down.” There was plenty of grass in that place, and they sat down (about five thousand men were there). 11 Jesus then took the loaves, gave thanks, and distributed to those who were seated as much as they wanted. He did the same with the fish.

12 When they had all had enough to eat, he said to his disciples, “Gather the pieces that are left over. Let nothing be wasted.” 13 So they gathered them and filled twelve baskets with the pieces of the five barley loaves left over by those who had eaten.

14 After the people saw the sign Jesus performed, they began to say, “Surely this is the Prophet who is to come into the world.” 

 

This parable is about the all-sufficiency of Jesus Christ to meet the vast needs of the world.   Christ uses inadequate people who surrender what they have to Him to meet the overwhelming needs of others.

 Christ is in control of every situation.

Jesus is in control of our physical, emotional and spiritual needs. During this difficult situation that the world is going through with Corona virus, with our scarce and inadequate medical resources, Jesus is there to help us. Let us trust in Him and commit our inadequacy to Him so that He will satisfy us with Peace, Hope, and good health until this COVID-19 tragedy has subsided.


JUMANNE TAREHE 28 APRILI 2020  ASUBUHI                                                

YOHANA 6:1-14

1 Baada ya hayo Yesu alikwenda zake ng'ambo ya Bahari ya Galilaya, nayo ndiyo ya Tiberia.
Na mkutano mkuu wakamfuata, kwa sababu waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa.
Naye Yesu akakwea mlimani, akaketi huko pamoja na wanafunzi wake.
Na Pasaka, sikukuu ya Wayahudi, ilikuwa karibu.
Basi Yesu alipoinua macho yake akaona mkutano mkuu wanakuja kwake, alimwambia Filipo, Tununue wapi mikate, ili hawa wapate kula?
Na hilo alilinena ili kumjaribu; kwa maana alijua mwenyewe atakalotenda.
Filipo akamjibu, Mikate ya dinari mia mbili haiwatoshi, kila mmoja apate kidogo tu.
Wanafunzi wake mmojawapo, Andrea, nduguye Simoni Petro, akamwambia,
Yupo hapa mtoto, yuna mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa?
10 Yesu akasema, Waketisheni watu. Na mahali pale palikuwa na majani tele. Basi watu waume wakaketi, wapata elfu tano jumla yao.
11 Basi Yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia walioketi; na kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka.
12 Nao waliposhiba, aliwaambia wanafunzi wake, Kusanyeni vipande vilivyobaki, kisipotee cho chote.
13 Basi wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili, vipande vya mikate mitano ya shayiri vilivyowabakia wale waliokula.
14 Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.

Huu ni mfano unaotuonesha utoshelevu ulio ndani ya Yesu Kristo, kwa mahitaji ya ulimwengu wote. Kristo hutumia uchache tulio nao ikiwa tutajisalimisha kwake ili aweze kukutana na mahitaji makubwa yanayotuzunguka.

 Yesu Kristo anao uweza juu ya mambo yote.

Yesu anao uweza juu ya hali zetu za kimwili, hisia zetu, na mahitaji yote ya kiroho. Katika kipindi hili kigumu ambacho dunia inapitia, juu ya janga hili la virusi vya Corona; kwa uchache wa rasilimali za afya tulizo nazo, Yesu yupo kutusaidia.  Imetupasa kumtumaini yeye na kukabidhi kwake vile vyote haba tulivyo navyo ili atutosheleze kwa Amani, Tumaini na afya njema nyakati zote hadi pale janga hili la COVID-19 litakapotoweka.