Date: 
28-03-2020
Reading: 
Joshua 5:10-12

SATURDAY 28TH MARCH 2020 MORNING JOSHUA 5:10-12 Joshua 5:10-12 New International Version (NIV)

10 On the evening of the fourteenth day of the month, while camped at Gilgal on the plains of Jericho, the Israelites celebrated the Passover. 11 The day after the Passover, that very day, they ate some of the produce of the land: unleavened bread and roasted grain. 12 The manna stopped the day after[d] they ate this food from the land; there was no longer any manna for the Israelites, but that year they ate the produce of Canaan.

When the people were able to provide for themselves from the rich produce of Canaan, God stopped the manna. God always provides; but He is perfectly free to change the source of His provision from time to time.  We only need to trust and obey Him.


JUMAMOSI TAREHE 28 MACHI 2020 ASUBUHI YOSHUA 5:10-12

10 Basi wana wa Israeli wakapanga hema zao huko Gilgali; nao wakala sikukuu ya pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi, jioni, katika nchi tambarare za Yeriko. 11 Nao wakala katika mazao ya nchi siku ya pili ya kuiandama hiyo sikukuu ya pasaka, mikate isiyotiwa chachu, na bisi, siku iyo hiyo. 12 Ndipo ile mana ikakoma siku ya pili yake, baada ya wao kuyala hayo mazao ya nchi; na hao wana wa Israeli hawakuwa na mana tena; lakini wakala katika viliwa vya nchi ya Kanaani mwaka huo.

 

Watu walipokuwa tayari kuzalisha chakula kwa ajili yao kutoka katika ardhi nzuri ya Kanaan, Mungu aliacha kuwapa mana. Mungu daima ni mpaji; hata hivyo anao uwezo wa kubadili njia anazotumia kututunza kulingana na wakati wake. Tunachohitaji kufanya ni kumwamini na kumtii tu.