Date: 
07-02-2022
Reading: 
Kutoka 33:18-23

Jumatatu asubuhi tarehe 07.02.2022

Kutoka 33:18-23

18 Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako.

19 Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la Bwana mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu.

20 Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi.

21 Bwana akasema, Tazama, hapa pana mahali karibu nami, nawe utasimama juu ya mwamba;

22 kisha itakuwa wakati unapopita utukufu wangu, nitakutia katika ufa wa ule mwamba, na kukufunika kwa mkono wangu hata nitakapokuwa nimekwisha kupita;

23 nami nitaondoa mkono wangu, nawe utaniona nyuma yangu, bali uso wangu hautaonekana.

Utukufu wa Mwana wa Mungu;

Katikati ya kazi ya kuwaongoza Israeli kuelekea nchi ya ahadi, Musa anaomba kuuona utukufu wa Mungu. Katika kulijibu hilo, Mungu anaahidi kumtendea wema na kumrehemu. Mungu anadhihirisha kuwa utukufu wake ni mkuu kiasi kwamba hakuna awezaye kuuona uso wake akaishi. Anaahidi kuwa na Musa mahali pote akakapopita.

Matendo ya Mungu kwetu hudhihirisha utukufu wake. Ni utukufu kwa sababu ni yeye awezaye kutuongoza katika njia sahihi zinazompendeza. Kama alivyomuahidi Musa, Mungu anatuongoza mahali pote tunapopita kwa utukufu wake. Anatutendea wema wakati wote. Wema wa Mungu husababisha tutende mema, na ndipo Mungu hutukuzwa. Tutauona utukufu wa Mungu tukikaa kwake na kutenda yatupasayo.

Tunakutakia wiki njema yenye Utukufu wa Mungu.