Date: 
16-06-2020
Reading: 
Matthew 16:24-27

TUESDAY 16TH JUNE 2020    MORNING                                               

Matthew 16:24-27 New International Version (NIV)

24 Then Jesus said to his disciples, “Whoever wants to be my disciple must deny themselves and take up their cross and follow me. 25 For whoever wants to save their life[f] will lose it, but whoever loses their life for me will find it. 26 What good will it be for someone to gain the whole world, yet forfeit their soul? Or what can anyone give in exchange for their soul? 27 For the Son of Man is going to come in his Father’s glory with his angels, and then he will reward each person according to what they have done.

We are called to "take up the cross," which rather clearly cannot mean anything but It is to risk danger and death at the hands of the judges and rulers of this world for the sake of witnessing the truth, the message of new life in Christ Jesus.

Jesus Christ asks you today, ‘will you heed my call to work for justice and peace, even if that brings you into conflict with the judges and rulers of this world, who have the power to put you to death?

Jesus is the rock upon which to build a secure, long, and productive life. Therefore, take care to obey God's word and God will take care of you.


JUMANNE TAREHE 16 JUNE 2020     ASUBUHI             

MATHAYO 16:24-27

24 Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.
26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
27 Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

 

Tunaitwa “kujitwika msalaba,” ambayo haimaanishi jambo jingine isipokuwa ni kujitoa maisha yetu katikati ya hatari na kifo kwenye mikono ya waamuzi na watawala wa dunia hii, kwa ajili ya kushuhudia kweli, yaani ujumbe wa maisha mapya katika Kristo Yesu.

Leo hii Yesu Kristo anakuuliza, ‘je, utafuata wito wangu wa kutenda haki na kuwa mpatanishi; hata kama itakufarakanisha na wakuu na watawala wa dunia hii, ambao wana nguvu na mamlaka ya kukuuwa?

Yesu ni mwamba ambao juu yake tunaweza kujenga maisha marefu, yaliyo salama, na yenye manufaa. Hivyo, uwe mwangalifu kulitii neno la Mungu na Mungu atakutunza.