Date: 
26-11-2022
Reading: 
Muhubiri 8:11-13

Jumamosi asubuhi tarehe 26.11.2022

Mhubiri 8:11-13

[11]Kwa sababu hukumu juu ya tendo baya haitekelezwi upesi, mioyo ya wanadamu huthibitishwa ndani yao ili kutenda mabaya.

[12]Ajapokuwa mwenye dhambi amefanya maovu mara mia, akazidisha siku zake; lakini hata hivyo najua hakika ya kwamba itakuwa heri kwao wamchao Mungu, wenye kicho mbele zake;

[13]walakini haitakuwa heri kwa mwovu, wala hatazidisha siku zake, zilizo kama kivuli; kwa sababu hana kicho mbele za Mungu.

Uzima wa ulimwengu ujao;

Tunasoma juu ya njia za Mungu katika kumkomboa mwanadamu. Somo linaonesha kwamba Mungu huwapa nafasi watendao dhambi kufanya toba. Tunasoma kwamba wanayo heri wamchao Bwana, lakini waovu hawana heri! Hivyo Bwana hapendi mtu yeyote apotee Petro alivyoandika;

2 Petro 3:9

[9]Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.

Tumepewa nafasi ya kumpokea Yesu, na kufanya toba wakati wote, maana Bwana anataka sote tutubu na kuurithi uzima wa milele. Tusiipoteze neema hii.

Tutubu dhambi zetu, Yesu akae kwetu siku zote, ili mwishoni tuurithi uzima wa milele kama alivyotuahidi.

Siku njema.