Ziara za kutembelea mitaa: Mchungaji Mzinga azuru mitaa ya Viwege na Tabora

Mtaa wa Tabora ni mmojawapo kati ya mitaa mitano inayotunzwa na Usharika wa Kanisa Kuu la Azaniafront Cathedral. Mtaa huo unapatikana katika wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani ukiwa na washarika takribani 120.

Miongoni mwa huduma za kichungaji zitolewazo kwenye mitaa inayotunzwa na Usharika wa Kanisa Kuu ni pamoja na kufungisha ndoa, ubatizo, ushiriki wa meza ya Bwana, kipaimara, kupokea wakristo wageni wanaotoka katika madhehebu mengine, kurudisha washarika kundini na kuhudumu katika sherehe mbalimbali zilizo katika kalenda ya kanisa.

Sikukuu ya Mikael na Watoto 2020 yafanyika Usharikani Azaniafront

"Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie kwa maana ufalme wa mbingu ni wao", hayo ni maneno ya kutoka katika Biblia yaliyotumika katika mahubiri yaliyofanyika katika ibada ya sikukuu ya Mikael na watoto iliyofanyika siku ya Jumapili tarehe 27 September 2020 katika Usharika wa Kanisa Kuu Azaniafront.

Sikukuu ya Mikael na watoto, hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kumkumbuka malaika Mikel na watakatifu wote pamoja na watoto. Ibada hii hufanyika kwa kuongozwa na watoto wakisaidiana na walimu wao pamoja na mtumishi wa usharika (parish worker).