Date: 
15-09-2025
Reading: 
Kumbukumbu la Torati 19:14

Jumatatu asubuhi tarehe 15.09.2025

Kumbukumbu la Torati 19:14

Usiiondoe alama ya mpaka wa jirani yako, waliouweka watu wa kale katika urithi wako, utakaorithi ndani ya nchi akupayo Bwana, Mungu wako, uimiliki.

Mtendee mema jirani yako;

Tunaanza juma jipya kwa kusoma Mungu akiwapa Israeli sheria kuhusu mipaka ya ardhi. Israeli wanaambiwa kwamba mtu asiuondoe mpaka wa jirani yake uliowekwa na watu wa kale katika urithi wake ambao atarithi ndani ya nchi apewayo na Bwana Mungu kuimiliki. Katika Torati hiyo hiyo, Mungu anaonesha kwamba kuondoa mpaka ni laana;

Kumbukumbu la Torati 27:17

Na alaaniwe aondoaye mpaka wa jirani yake. Na watu wote waseme, Amina.

Somo la asubuhi hii linahusu kutoondoa mpaka wa jirani. Bila shaka ililenga haki kwa wamiliki wote wa ardhi na ujirani mwema. Kwa zama za leo, lugha ya kutoondoa mpaka ni pana kwa maana ya kulenga majirani kukaa pamoja kwa upendo bila chuki na ugomvi. Yesu Kristo alitupa amri kuu ambayo ni upendo. Tukiishika amri hii, kila mmoja atamtendea mema jirani yake. Amina

Uwe na wiki njema

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com