DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 31 AGOSTI, 2025
SIKU YA BWANA YA 11 BAADA YA UTATU
NENO LINALOTUONGOZA NI
MUNGU HUWAPINGA WENYE KIBURI
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 24/08/2025
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 24/08/2025 ni Washarika 780 Sunday School 272
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Leo jumapili tarehe 31/08/2025 vijana wetu watacheza mchezo wa robo fainali na Vijana wa Kinyerezi. Uwanja wa Kentoni Mwenge karibu na TRA. Washarika tuendelee kuwaombea vijana wetu na tujitokeze kwa wingi kwenda kuwashangilia.
8. Leo jumapili tarehe 31/08/2025 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika karibuni.
9. Jumapili Ijayo tarehe 07/09/2025 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.
10. Uongozi wa Wajane na Wagane unapenda kuwatangazia Wajane na Wagane wote kuwa jumamosi ya tarehe 13/09/2025 kutakuwa na semina kuanzia saa 3.00 asubuhi mpaka saa 7.00 mchana hapa Kanisani Azania Front.
11. Kamati ya Ushirikiano na Habari inaendelea na maandalizi ya Washarika wa hapa Azania Front watakaokwenda Marekani mwezi ujao kwa mwaliko wa Usharika rafiki wa Messiah. Wawakilishi hawa ni kutoka Ibada zote tatu wakiwemo Wanawake, Wanaume, Vijana na Wazee; wakiongozwa na Mchungaji. Kamati imeona ni vema kuhakikisha Wawakilishi hao wana uelewa wa masuala ya msingi kuhusu Azania Front, hususan uhusiano wetu na Messiah; Kanisa nchini Tanzania, na pia Tanzania kama nchi. Hii itawawezesha kushiriki vema kwenye mzungumzo na wenyeji wao. Kwa maana hiyo, tungependa kuhimiza vikundi vyetu hapa Kanisani kutoa ushirikiano na vipende kutumia fursa hiyo kuwezesha Wawakilishi hao kwenda kuelezea kwa ufasaha huduma zinazotolewa na vikundi husika. Lengo ni kuonesha Kanisa linagusa vipi maisha ya Wakristo na jamii kwa ujumla. Vikundi vinaweza kutoa maelezo ya huduma zao, kutuma salamu au zawadi. Tafadahali wasiliana na: Mwenyekiti Mzee Cuthbert Swai au Katibu mzee Jaqueline Swai, au ofisi ya Mchungaji.
12. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 13.09.2025
SAA 6:00 MCHANA
Bw.Emanuel Joseaugusto Alexandre na Bi. Sania Martin Kasyanju
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 06.09.2025 AMBAYO ITAFUNGWA USHARIKA WA KKKT NJIA PANDA MOSHI KATI YA
-
Bw. Gift Godbless Mkony na Bi. Oneska James Mbwile
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
13. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Raymond Sangiwa
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Mruma
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa ………………………
- Kinondoni: Kwa ………………………….
- Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
- Oysterbay/Masaki: Kwa …………………………………………..
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bw & Bibi Kelvin Matandiko
- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Michael Nkya
14. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.