Date: 
10-06-2019
Reading: 
Psalm 80:7-11, John 7:37-39, Isaiah 41:14-18 (Zaburi 80:7-11, Yohana 7:37-39, Isaya 41:14-18)

MONDAY 10TH JUNE 2019 PENTECOST MONDAY.

THEME: THE SPREADING OF THE HOLY SPIRIT

Psalm 80:7-11, John 7:37-39, Isaiah 41:14-18

 

Psalm 80:7-11 New International Version (NIV)

Restore us, God Almighty;
    make your face shine on us,
    that we may be saved.

You transplanted a vine from Egypt;
    you drove out the nations and planted it.
You cleared the ground for it,
    and it took root and filled the land.
10 The mountains were covered with its shade,
    the mighty cedars with its branches.
11 Its branches reached as far as the Sea,[a]
    its shoots as far as the River.[b]

Footnotes:

  1. Psalm 80:11 Probably the Mediterranean
  2. Psalm 80:11 That is, the Euphrates

 

John 7:37-39 New International Version (NIV)

37 On the last and greatest day of the festival, Jesus stood and said in a loud voice, “Let anyone who is thirsty come to me and drink. 38 Whoever believes in me, as Scripture has said, rivers of living water will flow from within them.”[a] 39 By this he meant the Spirit, whom those who believed in him were later to receive. Up to that time the Spirit had not been given, since Jesus had not yet been glorified.

Footnotes:

  1. John 7:38 Or me. And let anyone drink 38 who believes in me.” As Scripture has said, “Out of him (or them) will flow rivers of living water.”

 

Isaiah 41:14-18 New International Version (NIV)

14 Do not be afraid, you worm Jacob,
    little Israel, do not fear,
for I myself will help you,” declares the Lord,

    your Redeemer, the Holy One of Israel.
15 “See, I will make you into a threshing sledge,
    new and sharp, with many teeth.
You will thresh the mountains and crush them,

    and reduce the hills to chaff.
16 You will winnow them, the wind will pick them up,
    and a gale will blow them away.
But you will rejoice in the Lord

    and glory in the Holy One of Israel.

17 “The poor and needy search for water,
    but there is none;
    their tongues are parched with thirst.
But I the Lord will answer them;

    I, the God of Israel, will not forsake them.
18 I will make rivers flow on barren heights,
    and springs within the valleys.
I will turn the desert into pools of water,

    and the parched ground into springs.

God promises to have mercy on His people Israel. He will bless them and restore them.  They will rejoice in God. They are thirsty and God will send them rivers of water to refresh the land.  Water is also used as a symbol of the Holy Spirit.

Jesus spoke to the Samaritan woman at the well and promised to give her living water.

Thank God that He cares for your Spiritual and your physical needs and He has given you the Holy Spirit to guide you.  


JUMATATU YA PENTECOSTE TAREHE 10 JUNI 2019

WAZO KUU: KUENEA KWA ROHO MTAKATIFU

Zaburi 80:7-11, Yohana 7:37-39, Isaya 41:14-18

Zaburi 80:7-11

Ee Mungu wa majeshi, uturudishe, Uangazishe uso wako nasi tutaokoka. 
Ulileta mzabibu kutoka Misri, Ukawafukuza mataifa ukaupanda. 
Ulitengeneza nafasi mbele yake, Nao ukatia mizizi sana ukaijaza nchi. 
10 Milima ilifunikwa kwa uvuli wake, Matawi yake ni kama mierezi ya Mungu. 
11 Nao uliyaeneza matawi yake hata baharini, Na vichipukizi vyake hata kunako Mto. 
 

Yohana 7:37-39

37 Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. 
38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. 
39 Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa. 
 

Isaya 41:14-18

14 Usiogope, Yakobo uliye mdudu, nanyi watu wa Israeli; mimi nitakusaidia, asema Bwana, na mkombozi wako ni Mtakatifu wa Israeli. 
15 Tazama, nitakufanya kuwa chombo kikali kipya cha kupuria, chenye meno; utaifikicha milima, na kuisaga; nawe utafanya vilima kuwa kama makapi. 
16 Utawapepeta, na upepo utawapeperusha; upepo wa kisulisuli utawatawanya; nawe utamfurahia Bwana, utajitukuza katika Mtakatifu wa Israeli. 
17 Maskini na wahitaji wanatafuta maji, wala hapana; ndimi zao zimekauka kwa kiu; mimi, Bwana, nitawasikia, mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha. 
18 Nitafunua vijito vya maji juu ya vilima, na chemchemi katikati ya mabonde; nitageuza jangwa kuwa ziwa la maji, na mahali pakavu kuwa vijito vya maji. 
 

Mungu anaahidi kuhurumia watu wake Israeli. Mungu atawainua. Mungu anajali mahitaji yao. Mungu atawapa furaha. Wanakiu na nchi inaukauka. Mungu atatoa chemchemi ya mito ya maji. Atakutana na kiu yao ya kimwili. Pia maji ni alama ya Roho Mtakatifu.

Yesu aliahidi kumpa Mama Msamarai kule kisimani Maji yaliyo hai, yaani Roho Mtakatifu.

Mshukuru Mungu anajali mahitaji yako ya kimwili na kiroho. Umepewa Roho Mtakatifu kuongoza maisha yako.