MATANGAZO YA USHARIKA 

LEO TAREHE 28 APRILI, 2024

SIKU YA BWANA YA 4 BAADA YA PASAKA

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

  NJOONI TUMWIMBIE BWANA 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 21/04/2024

4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

5. Leo tarehe 28/04/2024 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika karibuni

6. Jumapili ijayo tarehe 05/05/2024 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.

7. Jumapili ijayo tarehe 05/05/2024 tutakuwa na uimbaji wa Kantante Domino badala ya leo. Makabila yaliyojiandikisha wajiandae.

8. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 18/05/2024 ITAKAYOFUNGWA SAA 9.00 ALASIRI KATI YA

  • Bw. Emmanuel Hezron Mkonyi na Bi. Dianna Hardson Massawe

Tangazo hili limebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

9. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: Kwa ……………………………..
  • Mjini kati: ………………..
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Ruth Korosso
  • Kinondoni: Kwa Prof. Geofrey Mmari
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bw. na Bi. Buchanagandi.  
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Zebadiah Moshi siku ya Jumatano Mei Mosi saa 11 jioni.
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa …………………..
  • Oysterbay, Masaki: Kwa …………………….

10. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.