Date: 
08-11-2022
Reading: 
Ufunuo 4:1-16

Jumanne asubuhi tarehe 08.11.2022

Ufunuo wa Yohana 4:1-6

[1]Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo.

[2]Na mara nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti;

[3]na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi.

[4]Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu.

[5]Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo. Na taa saba za moto zilikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.

[6]Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma.

Sisi ni wenyeji wa mbinguni;

Yohana anafunuliwa juu ya ibada ya mbinguni kwa ajili ya watakatifu wote mbele ya kiti cha enzi. Yohana anaoneshwa kusanyiko likiwa mbele ya kiti cha enzi, tayari kwa ibada. Ibada hii ni kwa ajili ya wale waliokombolewa kwa damu ya Mwana kondoo, walioushinda ulimwengu. 

Tunakumbushwa kuwa baada ya maisha haya ipo siku ya hukumu, ambapo kila mmoja wetu atahukumiwa kwa kadri ya matendo yake. Nakualika asubuhi hii kutafakari kama utahudhuria ile ibada kuu ya mbinguni, na hii ni pale tu kama Yesu atafanyika kiongozi wako maisha yako yote.

Siku njema.