Date: 
11-02-2022
Reading: 
Yohana 17:4-9

Ijumaa asubuhi tarehe 11.02.2022

Yohana 17:4-9

4 Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.

5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.

6 Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika.

7 Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako.

8 Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.

9 Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako;

Utukufu wa Mwana wa Mungu;

Yohana sura ya 17 hutajwa kama sala ndefu ya Yesu aliyoommba (iliyoandikwa) alipoombea Kanisa lake umoja. Katika sala hiyo leo tunaona akimtukuza Baba, akiomba naye kutukuzwa kwa utukufu aliokuwa nao. Yesu anasema katika sala kuwa anao Utukufu.

Tunaitwa kutambua kuwa Yesu ndiye mwana wa Mungu, mwenye Utukufu. Tunao wajibu wa kumtukuza. Kumtukuza kunakofaa siyo maneno na mbwembwe za jukwaani, bali ni kuishi kwa kadri ya mapenzi yake, ili siku moja nasi tuingie mbinguni, kwenye Utukufu.

Siku njema.