Date: 
27-03-2020
Reading: 
1 Corinthians 11:23-28

FRIDAY 27TH MARCH 2020  MORNING                                              

1 Corinthians 11:23-28 New International Version (NIV)

23 For I received from the Lord what I also passed on to you: The Lord Jesus, on the night he was betrayed, took bread, 24 and when he had given thanks, he broke it and said, “This is my body, which is for you; do this in remembrance of me.” 25 In the same way, after supper he took the cup, saying, “This cup is the new covenant in my blood; do this, whenever you drink it, in remembrance of me.” 26 For whenever you eat this bread and drink this cup, you proclaim the Lord’s death until he comes.

27 So then, whoever eats the bread or drinks the cup of the Lord in an unworthy manner will be guilty of sinning against the body and blood of the Lord. 28 Everyone ought to examine themselves before they eat of the bread and drink from the cup. 

The Lord’s Supper reminds us of the atonement for our sins that Christ made possible through his death on the cross. Jesus wants us to observe this supper as a sacred rite and he require Christians to be considerate of each other’s needs.

This is how we know what love is: Jesus Christ laid down his life for us. And we ought to lay down our lives for our brothers and sisters {1John 3:16}.


IJUMAA TAREHE 27 MACHI 2020  ASUBUHI                           

1 WAKORINTHO 11:23-28

23 Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate,
24 naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.
25 Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.
26 Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.
27 Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana.
28 Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe.

Chakula cha Bwana au Ushirika Mtakatifu unatukumbusha jinsi Kristo alivyojitoa kufa msalabani ili awe fidia ya dhambi zetu. Yesu anataka tuitazame meza ya Bwana kama tendo takatifu na anataka Wakristo kujali mahitaji ya kila mmoja wetu. .

Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.{1Yohana 3:16}.