MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 01 JUNI, 2025

NENO LINALOTUONGOZA NI  

MUNGU HUSIKIA MAOMBI YETU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Wageni waliyeotufikia na cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 25/05/2025

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 18/05/2025 ni Washarika 797. Sunday School 152

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Leo tarehe 01/06/2025 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika karibuni.

8. Jumamosi ijayo tarehe 07/06/2025 saa 3.00 asubuhi Katika Usharika wa KKKT Mbezi Beach, kutakuwa na ibada maalum ya maombi kwa ajili ya waliohitimu kidato cha sita na wahitimu wengine. Ibada hii maalum inatambulika kama Mtoko wa Baba Askofu Dr. Alex Gehaz Malasusa. Neno kuu: KAMA SI BWANA ALIYEKUWA PAMOJA NASI, ISRAELI NA ASEME SASA. Vijana walio hitimu pamoja na wazazi wao wanaombwa kushiriki kikamilifu. Washiriki wote wafike ofisi ya Mchungaji ili kupata link ya kujiandikisha. Pia wazazi mnahimizwa kuwasajili pia watoto walioko shule za Bweni. 

9. Jumapili ijayo tarehe 08/06/2025 ni siku ya ubatizo wa watoto na kurudi kundini. Watakaohitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.

10. Uongozi wa Shule ya Jumapili unapenda kuwatangazia Wazazi/Walezi kuwa Tamasha la uimbaji la watoto litafanyika mwezi wa sita. Sare watakayovaa itakuwa ni tshirt ambazo zimeandaliwa na Uongozi wa DMP. Tshirt moja ni sh. 12,000/=. Hivyo Wazazi na Walezi mnaombwa muwanunulie watoto ili waweze kuvaa siku hiyo ya tamasha. Mungu awabariki.

11. NDOA. Hakuna Ndoa za Washarika

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa Matangazo karibu na duka letu la vitabu.

12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Watatangaziana
  • Upanga: Kwa Mama Waeli Koshuma
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa ……………………
  • Kinondoni: Kwa Prof. na Bibi S. Kulaba
  • Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
  • Oysterbay/Masaki: Kwa Mama Elipina Mlaki
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo
  • Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Kwa Mama Margaret Lema

13. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.

14. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili. Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.