Date: 
19-05-2020
Reading: 
1 Kings 3:1-9 (1 Wafalme 3:1-9)

TUESDAY 19TH MAY 2020      MORNING                                                           

1 Kings 3:1-9 New International Version (NIV)

3 Solomon made an alliance with Pharaoh king of Egypt and married his daughter. He brought her to the City of David until he finished building his palace and the temple of the Lord, and the wall around Jerusalem. The people, however, were still sacrificing at the high places, because a temple had not yet been built for the Name of the Lord. Solomon showed his love for the Lord by walking according to the instructions given him by his father David, except that he offered sacrifices and burned incense on the high places.

The king went to Gibeon to offer sacrifices, for that was the most important high place, and Solomon offered a thousand burnt offerings on that altar. At Gibeon the Lord appeared to Solomon during the night in a dream, and God said, “Ask for whatever you want me to give you.”

Solomon answered, “You have shown great kindness to your servant, my father David, because he was faithful to you and righteous and upright in heart. You have continued this great kindness to him and have given him a son to sit on his throne this very day.

“Now, Lord my God, you have made your servant king in place of my father David. But I am only a little child and do not know how to carry out my duties. Your servant is here among the people you have chosen, a great people, too numerous to count or number. So give your servant a discerning heart to govern your people and to distinguish between right and wrong. For who is able to govern this great people of yours?”

God is more ready to hear than we are to pray.  We are commanded to ask, and God is promising to give, because He loves to give; and  it is His nature to give. 

There is an amazing promise that God seems to offer Solomon whatever he wants. This was not only because Solomon sacrificed 1,000 animals. It was because his heart was surrendered to God. If we humble ourselves and surrender to Jesus, He will hear and answer our prayers.


JUMANNE TAREHE 19 MEI 2020    ASUBUHI                                              

1WAFALME 3:1-9

1 Huyo Sulemani akafanya ujamaa na Farao, mfalme wa Misri, akamwoa binti yake Farao, akamleta mjini mwa Daudi, hata alipokwisha kuijenga nyumba yake, na nyumba ya Bwana, na ukuta wa kuuzunguka Yerusalemu.
Ila watu walikuwa wakichinja dhabihu katika mahali pa juu, kwa sababu haikuwapo nyumba iliyojengwa kwa jina la Bwana, hata siku zile.
Sulemani naye akampenda Bwana, akienda katika amri za Daudi babaye, ila hutoa dhabihu na kufukiza uvumba katika mahali pa juu.
Basi mfalme akaenda Gibeoni, ili atoe dhabihu huko; kwa kuwa ndipo mahali pa juu palipo pakuu. Sulemani akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu ya madhabahu ile.
Na huko Gibeoni Bwana akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku; Mungu akamwambia, Omba utakalo nikupe.
Sulemani akasema, Umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu, kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na katika unyofu wa moyo pamoja nawe; nawe umemwekea na fadhili hii kubwa, maana umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo.
Na sasa, Ee Bwana, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia.
Na mtumwa wako yu katikati ya watu wako uliowachagua, watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala kufahamiwa idadi yao, kwa kuwa ni wengi.
Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?

Mungu yuko tayari kusikia zaidi ya jinsi tuombavyo. Mungu anatuagiza kuomba, na anaahidi kutupatia yale tuombayo kwa sababu anapenda kutoa; na ni asili yake kuwapa watoto wake mahitaji yao yote.

Hapa kuna ahadi ya kushangaza ambayo Mungu anampa Sulemani, kuomba lolote atakalo. Hii siyo kwa sababu mfalme Sulemani alitoa dhabihu ya wanyama 1,000; bali ni kwa sababu aliutoa moyo wake kwa Mungu. Ikiwa tutajinyenyekeza na kutoa mioyo yetu yote kwa Yesu, atasikia na kujibu maombi yetu.