Date: 
08-01-2021
Reading: 
1 PETER 2:9-10

FRIDAY 8TH JANUARY 2021 MORNING                                       

1 PETER 2:9-10 New International Version (NIV)

But you are a chosen people, a royal priesthood, a holy nation, God’s special possession, that you may declare the praises of him who called you out of darkness into his wonderful light. 10 Once you were not a people, but now you are the people of God; once you had not received mercy, but now you have received mercy.

A Christian is granted access to God through Jesus Christ; we can hear from His Word and talk to Him through prayer. In order to know the value of our faith, just remember that God chose us, undeserving sinners, as His representatives. He uses us to gather other sinners to Himself, through our lives and lips; to share the message of what God has done for us.


IJUMAA TAREHE 8 JANUARY 2021  ASUBUHI                        

1 PETRO 2:9-10

Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.

Mkristo amepewa kibali cha kuwasiliana na Mungu kupitia Yesu Kristo; na tunaweza kumsikiliza kupitia neno lake na kuzungumza naye kwa njia ya maombi. Tukitaka kujua thamani ya wokovu wetu, tukumbuke kuwa Mungu alituchagua, wenye dhambi tusiostahili, kuwa mabalozi wake. Ametuweka sisi kuwaita wenye dhambi wamrudie yeye; kwa njia ya maisha na vinywa vyetu; kuyashuhudia yale Mungu aliyotutendea.