Date: 
11-08-2022
Reading: 
1 Yohana 5:18-21

Alhamisi asubuhi tarehe 11.08.2022

1 Yohana 5:18-21

[18]Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi.

[19]Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu.

[20]Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.

[21]Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu.

Mlango wa kuingia mbinguni;

Yohana anamalizia waraka wake wa kwanza kwa kuwajulisha wasomaji wake kuwa kwa kumwamini Yesu, wanao uzima wa milele. Ni katika hilo anawasihi kujilinda na mwovu shetani ili wasianguke dhambini. Yohana anakazia kuwa Yesu Kristo ndiye Mungu kweli aliyewapa akili wamjue yeye na kumwamini.

Ujumbe wa Yohana asubuhi ni kuwa tuwe na ujasiri katika Yesu tuliyempokea na kumwamini, tukiamini kuwa kwa kumfuata tunao uzima wa milele. Tujilinde nafsi zetu dhidi ya dunia hii tukitenda mema, ili Yesu Kristo aliye mlango wa kuingia mbinguni atupe uzima wa milele.

Siku njema.