Date: 
06-08-2022
Reading: 
1Wakorintho15:9-11

Jumamosi asubuhi tarehe 06.08.2022

1 Wakorintho 15:9-11

9 Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mitume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu.

10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.

11 Basi, kama ni mimi, kama ni wale, ndivyo tuhubirivyo, na ndivyo mlivyoamini.

Mungu amejaa neema inayotuwezesha;

Mtume Paulo anasimulia alivyokuwa mbaya akilitesa Kanisa. Kwa aliyotenda zamani anaonesha kuwa hakustahili, ila kwa neema ya Mungu alibadilika na kuhubiri injili. Anaonesha jinsi Yesu alivyowatokea mitume baada ya ufufuko, hadi yeye. Anaona kutokewa na Yesu kwake ni neema kubwa sana.

Kumbe Yesu hachagui, na neema yake ni kwa wote. Hata wasiomwamini, wakimjia huwapokea. Kama alivyomuita Paulo, ametuita na sisi, akitukumbusha kukaa kwake kwenye neema kuu.

Jumamosi njema.