Date: 
04-02-2022
Reading: 
2 Timotheo 4:16-18

2 Timotheo 4:16-18

16 Katika jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo.
17 Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba.
18 Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.

Tunalindwa na nguvu za Mungu;

Mtume Paulo anaonekana kukiri ukuu wa Mungu, akiwaombea msamaha wale waliokuwa tofauti naye wakati wa shida katika huduma yake. Mungu alimuokoa katika shida, na anazidi kuomba neema ya Mungu ili aweze kuufikia uzima  wa milele.

Paulo anaonesha kumtegemea Mungu katika huduma yake, wakati wa shida na raha. 
Huu ni ujumbe kwetu, kumtegemea Mungu wakati wa  shida na raha, ili nasi tuufikie uzima wa milele. Itawezekana, maana tunalindwa na nguvu za Mungu.


Siku njema.