Date: 
22-07-2020
Reading: 
2CORINTHIANS 7:5-10 (2Wakorintho 7:5-10)

WEDNESDAY 22ND  JULY 2020   MORNING                                    

2CORINTHIANS 7:5-10 (NIV)

For when we came into Macedonia, we had no rest, but we were harassed at every turn—conflicts on the outside, fears within. But God, who comforts the downcast, comforted us by the coming of Titus, and not only by his coming but also by the comfort you had given him. He told us about your longing for me, your deep sorrow, your ardent concern for me, so that my joy was greater than ever.

Even if I caused you sorrow by my letter, I do not regret it. Though I did regret it—I see that my letter hurt you, but only for a little while— yet now I am happy, not because you were made sorry, but because your sorrow led you to repentance. For you became sorrowful as God intended and so were not harmed in any way by us. 10 Godly sorrow brings repentance that leads to salvation and leaves no regret, but worldly sorrow brings death.

It is not our sorrow that cleanses us from sin, but Jesus’ blood.  It is the goodness of God that leads a man to repentance. Repentance means to turn around, and it takes diligence to stay turned around.  It is a change of purpose and intentions, a change of direction and action.


JUMATANO TAREHE 22ND JULAI 2020   ASUBUHI                       

2WAKORINTHO 7:5-10

Kwa maana hata tulipokuwa tumefika Makedonia miili yetu haikupata nafuu; bali tulidhikika kote kote; nje palikuwa na vita, ndani hofu.
Lakini Mungu, mwenye kuwafariji wanyonge, alitufariji kwa kuja kwake Tito.
Wala si kwa kuja kwake tu, bali kwa zile faraja nazo alizofarijiwa kwenu, akituarifu habari ya shauku yenu, na maombolezo yenu, na bidii yenu kwa ajili yangu, hata nikazidi kufurahi.
Kwa sababu, ijapokuwa naliwahuzunisha kwa waraka ule, sijuti; hata ikiwa nalijuta, naona ya kwamba waraka ule uliwahuzunisha, ingawa ni kwa kitambo tu.
Sasa nafurahi, si kwa sababu ya ninyi kuhuzunishwa, bali kwa sababu mlihuzunishwa, hata mkatubu. Maana mlihuzunishwa kwa jinsi ya Mungu, ili msipate hasara kwa tendo letu katika neno lo lote.
10 Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.

Hatuoshwi dhambi zetu kwa sababu ya huzuni zetu, bali kwa damu ya Yesu. Ni wema wa Mungu ndiyo unaomvuta mtu katika toba ya kweli. Toba maana yake ni kugeuka, na inahitaji juhudi ili kukaa katika uelekeo sahihi. Kutubu ni kuwa na mabadiliko katika malengo na makusudi; na ni mabadiliko yanayoleta uelekeo na matendo mapya.