Date: 
14-07-2020
Reading: 
2Timothy 2:11-13

TUESDAY 14TH JULY 2020    MORNING                                               

2Timothy 2:11-13 New International Version (NIV)

11 Here is a trustworthy saying:

If we died with him,
    we will also live with him;
12 if we endure,
    we will also reign with him.
If we disown him,
    he will also disown us;
13 if we are faithless,
    he remains faithful,
    for he cannot disown himself.

 

Christian can stand faithful as God empowers them. Even if one of us has been wavering, we still have time as the Spirit of God calls us even now, to turn back to the faithful God. We can be like the prodigal son, who came to his senses, saw his faithfulness, and came home to his father who had been faithful to him the whole time.


JUMANNE TAREHE 14 JULAI 2020     ASUBUHI             

2TIMOTHEO 2:11-13

11 Ni neno la kuaminiwa. Kwa maana, Kama tukifa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia;
12 Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi;
13 Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.

Mkristo anaweza kusimama kwa uaminifu  kadiri Mungu anavyomtia nguvu. Hata ikiwa mmoja wetu amekuwa mwenye kusita, bado tunao muda kwa kuwa Roho Mtakatifu wa Mungu anatuita hata sasa, kumgeukia Mungu aliye mwaminifu. Sisi tuwe kama mwana mpotevu, aliyetafakari moyoni mwake, akauona uaminifu wake; na kurudi nyumbani kwa baba yake ambaye alikuwa mwaminifu kwake wakati wote.