Date: 
16-01-2020
Reading: 
Acts 10:44-48 [Matendo 10:44-48]

THURSDAY 16TH JANUARY 2020  MORNING           

Acts 10:44-48 New International Version (NIV)

44 While Peter was still speaking these words, the Holy Spirit came on all who heard the message. 45 The circumcised believers who had come with Peter were astonished that the gift of the Holy Spirit had been poured out even on Gentiles. 46 For they heard them speaking in tongues[b] and praising God.

Then Peter said, 47 “Surely no one can stand in the way of their being baptized with water. They have received the Holy Spirit just as we have.” 48 So he ordered that they be baptized in the name of Jesus Christ. Then they asked Peter to stay with them for a few days.

The Holy Spirit's presence was the evidence that opened the way for baptism; and the evidence of their salvation.  The baptism in the Holy Spirit is for us today.  Let us always seek His powerful presence in our lives and ministries.


ALHAMISI TAREHE 16 JANUARI 2020  ASUBUHI     

MATENDO YA MITUME 10:44-48

44 Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno.
45 Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.
46 Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu,
47 Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?
48 Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha.

Kushuka kwa Roho Mtakatifu kulifungua njia ili watu wabatizwe; na ilikuwa ni uthibitisho wa wokovu wao. Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni wetu sisi Wakristo wa leo. Tutafute daima uwepo wa nguvu zake katika maisha yetu na huduma zetu.