Date: 
08-08-2022
Reading: 
Ayubu 28:23-28

Jumatatu asubuhi tarehe 8.08.2022

Ayubu 28:23-28

[23]Mungu ndiye aijuaye njia yake, 

Naye anajua mahali pake.

[24]Maana anatazama hata miisho ya nchi, 

Na kuona chini ya mbingu nzima.

[25]Apate kuufanyia upepo uzito wake; 

Naam, anayapima maji kwa kipimo.

[26]Hapo alipoiwekea mvua amri, 

Na njia kwa umeme wa radi.

[27]Ndipo alipoiona na kuitangaza; 

Aliithibitisha, naam, na kuichunguza.

[28]Kisha akamwambia mwanadamu, 

Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, 

Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.

Mlango wa kuingia mbinguni;

Ayubu baada ya kujaribiwa na shetani akipata mateso makali na kupoteza kila kitu, aliedelea kumcha Bwana. Na katika kumcha Bwana huko, sura ya 23 inaandika Yeremia akionesha hekima inapopatikana. Anaonesha kuwa hekima haipatikani popote, bali kwa Bwana kama mstari wa 28 unavyosema;

Ayubu 28:28

[28]Kisha akamwambia mwanadamu, 
Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, 
Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.

Hekima hutufanya kuwa kuwaza kwa usahihi, hivyo kunena na kutenda kwa usahihi. Hekima hii ilimuongoza Ayubu kukaa kwa Bwana pamoja na shida alizopata. Kumbe hekima ya Mungu ndiyo itasababisha tutende mema na kuuona mlango wa kuingia mbinguni.

Nakutakia wiki njema.