Date: 
24-08-2022
Reading: 
Esta 4:14-17

Jumatano asubuhi tarehe24.08.2022

Esta 4:14-17

[14]Kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na wokovu kwa njia nyingine; ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; walakini ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo?

[15]Basi Esta akawatuma ili wamjibu Mordekai,

[16]Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.

[17]Basi Mordekai akaenda zake, akafanya yote kama vile Esta alivyomwagiza.

Tutumie vizuri nafasi tuliyopewa;

Mfalme Ahasuero alimpandisha cheo Hamani kuwa juu ya maakida wote. Miongoni mwa watumishi wake, Modekai hakumsujudia huyo Hamani. Hamani alichukia hadi kutangaza kuwaua Wayahudi wote (jamii ya Modekai). Modekai akamtumia ujumbe Esta (myahudi) aliyekuwa Malkia kuwaokoa na kuuawa. Esta alifanikisha jambo hili.

Esta alitumia vizuri nafasi aliyopewa kuwaokoa Wayahudi wenzake. Haikuwa rahisi, lakini aliweza. 

Esta ni alama ya watu ambao wanatumia vema nafasi zao kuwasaidia wengine. Kumbe nasi tunaalikwa kutimiza wajibu wetu pale tulipo, kwa Utukufu wa Mungu. Ukiwa mahali ukafanya kazi isiyosaidia watu unakuwa huwafai watu, bali kujifaa mwenyewe. Unaweza kujifaa mwenyewe kumbe unajipoteza kama ambavyo Esta angenyamaza, naye angekufa maana alikuwa Myahudi. 

Unatumiaje nafasi yako?