Date: 
08-02-2022
Reading: 
Ezekiel 12:21-28

Jumanne asubuhi tarehe 08.02.2021

Ezekieli 12:21-28

21 Neno la Bwana likanijia, kusema,

22 Mwanadamu, ni mithali gani hii mliyo nayo katika nchi ya Israeli, mkisema, Siku hizo zinakawia na maono yote hayatimizwi.

23 Basi uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Nitaikomesha mithali hii, wasiitumie tena kama mithali katika Israeli; lakini uwaambie, Siku hizo ni karibu, na utimilizo wa maono yote.

24 Kwa maana hayatakuwapo tena maono yo yote ya ubatili, wala ubashiri wa kujipendekeza, katika nyumba ya Israeli.

25 Maana mimi ni Bwana; mimi nitanena, na neno lile nitakalolinena litatimizwa; wala halitakawilishwa tena; maana katika siku zenu, Ewe nyumba iliyoasi, nitalinena neno hilo na kulitimiza, asema Bwana MUNGU.

26 Neno la Bwana likanijia tena, kusema,

27 Mwanadamu, tazama, hao wa nyumba ya Israeli husema, Maono hayo ayaonayo ni ya siku nyingi zijazo, naye anatabiri habari ya nyakati zilizo mbali sana.

28 Basi uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Maneno yangu hayatakawilishwa tena hata moja, bali neno nitakalolinena litatimizwa, asema Bwana MUNGU.

Utukufu wa Mwana wa Mungu;

Israeli waliona ahadi za Bwana kwao zikikawia, lakini kupitia kwa nabii Ezekieli Bwana alithibitisha kuwa siku za kutimiza ahadi zake kwao zilikuwa karibu. Hata tabiri za manabii zilionekana ni za miaka mingi, lakini Mungu aliahidi kuwa zingetimizwa.

Ahadi za Bwana ni timilifu. Yeye hachelewi. Yesu alikufa, akazikwa, akafufuka na kupaa katika Utukufu wake. Kwa utukufu huo huo atarudi. Usione kurudi kwake kuwa mbali, ni karibu. Wajibu wetu ni kujiandaa ili ajapo kwa utukufu asituache.

Siku njema.