Date: 
13-04-2021
Reading: 
Ezekieli 37:12-14

JUMANNE TAREHE 13 APRILI 2021, ASUBUHI

Ezekieli 37:12-14

12 Basi tabiri, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitafunua makaburi yenu, na kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu, enyi watu wangu, nami nitawaingizeni katika nchi ya Israeli.
13 Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapoyafunua makaburi yenu, na kuwatoa ninyi katika makaburi yenu, enyi watu wangu.
14 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, nanyi mtaishi, nami nitawawekeni katika nchi yenu, nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, nimesema hayo, na kuyatimiza, asema Bwana.

Yesu ajifunua kwetu;

Nabii Ezekieli anatumwa kuleta ujumbe wa baraka kwa wote waaminio, ambapo Bwana anaahidi kuwabariki. Bwana anaahidi kuwapa Roho Mtakatifu, katika kutimiza ahadi zake, akisisitiza watu waendelee kuishi katika yeye.

Ezekieli anatupa ujumbe huu, tunapotafakari jinsi Yesu anavyojifunua kwetu. Yesu alikwisha kuahidi kuwa nasi hadi mwisho wa dahari. Hivyo tunaitwa kuishi ndani yake, naye ndani yetu, ili baraka yake iwe nasi siku zote kuelekea uzima wa milele.

Siku njema.


TUESDAY 13TH APRIL 2021, MORNING

Ezekiel 37:12-14, New International Version

12 Therefore prophesy and say to them: ‘This is what the Sovereign Lord says: My people, I am going to open your graves and bring you up from them; I will bring you back to the land of Israel. 13 Then you, my people, will know that I am the Lord, when I open your graves and bring you up from them. 14 I will put my Spirit in you and you will live, and I will settle you in your own land. Then you will know that I the Lord have spoken, and I have done it, declares the Lord.’”

Read full chapter

The prophet Ezekiel is sent to bring a message of blessing to all believers, where the Lord promises to bless them. The Lord promises to give them the Holy Spirit, in fulfillment of His promises, urging people to continue living in Him.

Ezekiel gives us this message, as we reflect on how Jesus reveals Himself to us. Jesus had promised to be with us until the end of time. Thus we are called to live in him, and he in us, so that his blessing may be with us always toward eternal life.