Date: 
27-08-2020
Reading: 
Hebrews 11:25-29 ( Waebrania 11:25-29)

THURSDAY 27TH AUGUST 2020 MORNING            

Hebrews 11:25-29 New International Version (NIV)

25 He chose to be mistreated along with the people of God rather than to enjoy the fleeting pleasures of sin. 26 He regarded disgrace for the sake of Christ as of greater value than the treasures of Egypt, because he was looking ahead to his reward. 27 By faith he left Egypt, not fearing the king’s anger; he persevered because he saw him who is invisible. 28 By faith he kept the Passover and the application of blood, so that the destroyer of the firstborn would not touch the firstborn of Israel.

29 By faith the people passed through the Red Sea as on dry land; but when the Egyptians tried to do so, they were drowned.

It’s easy to trust God when the sea is parting, when the walls of Jericho are falling, when His voice is clearly coming through to our spirit. But what about those days when God is silent? Think about God’s timing. Can we still trust in Him and wait?


ALHAMISI TAREHE 27 AGOSTI 2020  ASUBUHI     

WAEBRANIA 11:25-29

25 akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo;
26 akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.
27 Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana.
28 Kwa imani akaifanya Pasaka, na kule kunyunyiza damu, ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao.
29 Kwa imani wakapita kati ya Bahari ya Shamu, kama katika nchi kavu; Wamisri walipojaribu kufanya vivyo wakatoswa.

Ni rahisi kumwamini Mungu pale bahari inapogawanyika, wakati kuta za Yeriko zinapoanguka, na wakati ule tunapoisikia wazi sauti yake ikisema nasi mioyoni mwetu. Lakini inakuwaje katika siku zile Mungu anapokuwa kimya? Tafakari kuhusu wakati wa Mungu. Je, tunaweza kuendelea kumwamini na kusubiri?