Date: 
25-09-2021
Reading: 
Hesabu 14:18-19

JUMAMOSI TAREHE 25 SEPTEMBA 2021, ASUBUHI

Hesabu 14:18-19

18 BWANA ni mpole wa hasira, mwingi wa rehema, mwenye kusamehe uovu na makosa, naye hatamfanya mwenye hatia kuwa hana makosa kwa njia yo yote; mwenye kuwapatiliza wana kwa uovu wa baba zao, katika kizazi cha tatu na cha nne.

19 Nakusihi, usamehe uovu wa watu hawa, kama ukuu wa rehema yako ulivyo, kama ulivyowasamehe watu hawa, tangu huko Misri hata hivi sasa.

Huruma ya Mungu;

Musa alikuwa mbele za Mungu akiomba msamaha kwa ajili ya wana wa Israeli, Mungu asiwaangamize. Musa anamkumbusha Mungu maneno yake mwenyewe kuwa hana hasira na mwingi wa rehema, anayesamehe uovu (18). Mungu alimsikia Musa akawasamehe;

Hesabu 14:20

20 BWANA akasema, Mimi nimewasamehe kama neno lako lilivyokuwa;

Maisha tunayoishi yana mambo mengi yanayoweza kusababisha tukamkosea Mungu, kwa kujua na wakati mwingine tusijue. Musa anatukumbusha kwenda mbele  za Mungu kwa toba, na Mungu wa rehema hutusamehe.

Siku njema.