Date: 
03-02-2020
Reading: 
Isaiah 8:19-22

MONDAY 3RD FEBRUARY 2020  MORNING                                                         

Isaiah 8:19-22 New International Version (NIV)

19 When someone tells you to consult mediums and spiritists, who whisper and mutter, should not a people inquire of their God? Why consult the dead on behalf of the living? 20 Consult God’s instruction and the testimony of warning. If anyone does not speak according to this word, they have no light of dawn. 21 Distressed and hungry, they will roam through the land; when they are famished, they will become enraged and, looking upward, will curse their king and their God. 22 Then they will look toward the earth and see only distress and darkness and fearful gloom, and they will be thrust into utter darkness.

Because God is very jealous and possessive over His own children, He wants all of us to come directly to Him if we have any problems with our future, or what He might have in store for us in our future. 


JUMATATU TAREHE 3 FEBRUARI 2020  ASUBUHI                                          

ISAYA 8:19-22

19 Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong'ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?
20 Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.
21 Nao watapita katikati yake, wamedhikika sana na kuwa na njaa; na itakuwa watakapoona njaa, watalalamika na kuapa kwa mfalme wao, na kwa Mungu wao, na kuelekeza nyuso zao juu;
22 nao wataiangalia nchi, na, tazama, shida na giza; hapana changamko kwa sababu ya dhiki; nao watafukuzwa na kuingia katika giza kubwa.

Kwa kuwa Mungu ni mwenye wivu sana juu ya watoto wake, anatutaka sisi sote kumwendea yeye moja kwa moja ikiwa tuna hitaji lolote kuhusiana na mambo yajayo; au kuhusu yale aliyoandaa kwa ajili yetu.